Wabunge wawapongeza watoto wa Kikwete, Nkamia Saturday, July 01, 2017 Wanafunzi watatu walioshinda tuzo ya Genius Olympiad huko Marekani wametambulishwa bungeni jana kwa kuliletea Taifa heshima. Wanafunzi hao kutoka Sekondari ya Wavulana ya Feza jijini Dar es Salaam waliambatana na walimu wao wawili. Walikuja bungeni kwa mwaliko wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako. Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwatambulisha wageni watano wa Profesa Ndalichako wakiwamo walimu wawili na wanafunzi watatu walioshinda medali za dhahabu katika mashindano ya kimataifa ya mazingira na sayansi yaliyofanyika. “Tunawapongeza kwa kushinda tuzo hizo. Mmepeperusha bendera ya Tanzania vizuri sana,” alisema Ndugai. Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Abdallah Rubeya, Abdularazak Juma Nkamia ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia na Khalifan Jakaya Kikwete, mtoto wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete. Hakusita kutania na kuwapongeza wazazi wa watoto hao kwa...