Skip to main content

JPM ASEMA HAYA!!!!!!!!!!!

JPM Aagiza kukamatwa wanaongea ongea ovyo kuhusu Kibiti


Rais Magufuli amewaonya baadhi ya wanasiasa na kuwataka kufunga midomo yao wakati serikali inafanya kazi yake, Rais Magufuli amesema hayo leo wakati anazindua upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam.


Rais Magufuli amewataka wanasiasa kuzungumza mambo wanayoyajua lakini si kuongea ongea tu vitu ambavyo hawavifahamu na kusisitiza kuwa baadhi ya watu ambao serikali inawashikilia katika vyombo vya usalama wanahusika na mauaji ambayo yanatokea mkoani Pwani.


"Lakini niwaombe pia na wanasiasa ambao wameshindwa ku 'contol' midomo yao na muda mwingine wanazungumza hata vitu wasivyovijua, unakuta mwanasiasa anasema watu wamekaa sana rumande anashindwa kuelewa Marekani wale watu wabaya walikaa Guantanamo miaka na miaka, lakini kwetu wanaposhikwa watu ambao wanahusika na mambo ya ajabu katika nchi kuna watu wanaongea ongea. Pwani kuna watu wamekufa kule zaidi ya 35 askari zaidi ya 15 na wanaohusika na vifo hivyo ni pamoja na hao waliopo rumande lakini mtu anatoka anasema watu wamekaa mno, unaweza kuona huyo mtu naye anahusika kwa namna moja au nyingine, wasitufanye tukafika hapo sababu wataumia, wajifunze kufunga midomo yao wakati serikali inafanya kazi yake" alisisitiza Rais Magufuli. 


Rais Magufuli anasema kumekuwa na mzaha kwa baadhi ya watu kutokana na kuhongwa pesa ndiyo maana wao kazi yao ni kupinga kila kitu. 


"Mimi nimetuma ujumbe huu ili uwafikie Watanzania na waelewe, tuna mambo makubwa tunashughulikia katika nchi hii, lakini kumekuwa na mzaha mzaha tu, unakuta muda mwingine mnashughulikia rasilimali za watanzania zinavyoibiwa , lakini unakuta mtu mwingine anapinga hadharani kwa sababu amepewa vijisenti, ninawaomba watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao tutangulize masilahi ya nchi mbele, hujasimama hata siku moja kulaani mauaji yanayotokea huko halafu unaibuka unataka sifa za kisiasa eti hawa watu waachiwe, na bahati mbaya watu wanaokufa ni wa chama kimoja tu, nataka polisi mfanye kazi yenu."alisema Rais Magufuli 


Mbali na hilo Rais Magufuli amewataka polisi kuwakamata watu wote ambao wanaongea ongea juu ya mambo hayo ili walisaidie jeshi la polisi katika upelelezi, bila kuwaogopa kwa sura, wala mwendo wao.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO KUMI YA KUFANYA KABLA YA MIAKA 25

1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusagusa.   2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha. 3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwa wazazi au kupanga na nyumba na washkaji. 4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote! 5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi kuu-maintain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana. 6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia. 7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo. 8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza. 9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto. 10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya. Mwajuma huna mpango naye, achana naye. Acha kurudi rudi nyuma!

JE UNAMJUA ALIYETUNGA WIMBO WA TAIFA? HUYU APA

HUYU NDIYE MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA WA TANZANIA JE, unamfahamu mtu aliye tunga sauti (melody ) ya wimbo ambao leo Watanzania wanaiita Wimbo wa Taifa? Huyu ni Enock Sontonga , raia wa Afrika Kusini, aliye tunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ i Afrika’. Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905. Sauti ya wimbo huo u metumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za  Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania ambapo Tanzania na Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii. Nchi zingine tatu za Wazimbabwe , Nami bia na Afrika Kusini imetungwa nyimbo nyingine. Wimbo huu ulitungwa mwaka 1897  na kurekebishwa na wahariri mbalimbali mpaka kufikia kutumika vyema katika maswala ya kitaifa.

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6.  Hii itamsaidia kujua l