Skip to main content



MABINGWA wa Kombe la SportPesa, Gor Mahia kutoka Kenya wanatarajia kuikaribisha Everton FC inayoshiriki Ligi Kuu England katika mechi ya kirafiki itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam-

huku mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wa Tanzania.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, jana aliongoza viongozi mbalimbali wa serikali na wadau wa soka nchini waliojitokeza kuipokea timu hiyo ambayo imekuja nchini kwa mwaliko wa Kampuni ya SportPesa Tanzania.

Mechi ya leo itakuwa ni ya kwanza kwa Rooney tangu arejee katika klabu yake hiyo akitokea Manchester United ambayo aliitumikia kwa miaka 13.

Kocha wa Everton, Ronald Koeman, alisema kuwa kila mchezaji wa timu hiyo ambaye amekuja nchini atapata muda wa kucheza kuanzia dakika 45 na wataondoka kesho.

"Hii ndiyo mechi ya kwanza ya kirafiki na kila mchezaji nitampatia dakika 45. Tunacheza mpira kwa ajili ya kushindana, tunatarajia kupata ushindi katika mchezo huu utakaofanyika Tanzania," alisema.

Kocha Mkuu wa Gor Mahia, Dylan Kerr, alisema jana kuwa timu yake imejipanga kuitumia vizuri nafasi ya kucheza na Everton ambayo ina wachezaji wanaoshiriki moja ya ligi zenye kiwango cha juu duniani.

“Ninatumaini tutatumia vizuri nafasi hii kama ambavyo tulionyesha uwezo wetu na kuibuka washindi katika mashindano ya Kombe la SportPesa, hakuna timu ndogo katika dunia ya sasa, mpira ni uwanjani na si jina au taifa la mchezaji linalohusika kwenye mchezo,” alisema Kerr, kocha wa zamani wa Simba.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema jana kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na waamuzi wa hapa nchini wakiongozwa na Israel Nkongo, Fredinand Chacha na Frank Komba ambao wana beji zinazotambulika na Fifa ndiyo watachezesha mechi hiyo.

Alimtaja Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ndiye atakuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo inayotarajiwa kuanza saa 11:00 jioni
huku kiingilio cha chini kikiwa ni Sh. 3,000.kemege.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO KUMI YA KUFANYA KABLA YA MIAKA 25

1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusagusa.   2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha. 3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwa wazazi au kupanga na nyumba na washkaji. 4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote! 5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi kuu-maintain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana. 6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia. 7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo. 8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza. 9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto. 10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya. Mwajuma huna mpango naye, achana naye. Acha kurudi rudi nyuma!

JE UNAMJUA ALIYETUNGA WIMBO WA TAIFA? HUYU APA

HUYU NDIYE MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA WA TANZANIA JE, unamfahamu mtu aliye tunga sauti (melody ) ya wimbo ambao leo Watanzania wanaiita Wimbo wa Taifa? Huyu ni Enock Sontonga , raia wa Afrika Kusini, aliye tunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ i Afrika’. Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905. Sauti ya wimbo huo u metumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za  Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania ambapo Tanzania na Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii. Nchi zingine tatu za Wazimbabwe , Nami bia na Afrika Kusini imetungwa nyimbo nyingine. Wimbo huu ulitungwa mwaka 1897  na kurekebishwa na wahariri mbalimbali mpaka kufikia kutumika vyema katika maswala ya kitaifa.

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6.  Hii itamsaidia kujua l