Miongoni mwa kauli ambazo nilikuwa nasikia wakati nakua nilikuwa nasikia wanasema maisha ni kama kioo ukicheka na yenyewe yanacheka. Kwa kipindi hicho sikuwahi kujua wanamaana gani watu waliyokuwa wanasema hivyo. Ila kwa bahati nzuri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ninavyoelewa walikuwa wanamaanisha nini. Kwa utafiti wangu nimegundua ya kwamba katika maisha ya kusaka mafanikio ni lazima ujishughulishe kwa kutumia nguvu, kipaji, juhudi na maarifa ili uweze kupata mafanikio hayo. Na endapo utafanya kinyume chache utazidi kulaumu na kuishia kusema ndoto zangu ni kuwa mtu fulani na vitu kama hivyo. Mwandishi mmoja anayeitwa Charles Nduku aliwahi kuandika katika kitabu chake cha ‘my plan, my life’ kwa kusema acha Kuota ndoto bali anza kufanya. Kwa kipindi kirefu umekuwa unasema nataka kuwa hivi na vile. Kumbuka ya kwamba huu sio mda wa kusema maneno hayo. Ila muda wakuanza kutekeleza malengo yako. Watu wengi wapo vizuri zaidi kwa kusema kuliko kutenda, na ukichunguza vi...
This is Blog aim at give the update information on the real life and leads to acknowledge the individual with the knowledge and skills on the different phenomena like technology, business, education and relationship