Skip to main content

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke.

Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo. 

Nani anaweza kutumia njia ya kalenda
Moja, Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo.

Pili, Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki.

Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana. 
Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6.  Hii itamsaidia kujua lini mayai yake yalipevuka.  Njia hii inamsaidia zaidi mwanamke aliye na mzunguko wa hedhi wa siku 28, na hutegemea kufahamu kuwa yai la mwanamke hupevuka siku 14 kabla hajaingina kwenye hedhi.

 Kwa mfano;
1. Kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 1 Juni (na una mzunguko wa hedhi wa siku 28), basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 29 Juni.  Kwa hiyo yai lako litapevuka siku 14 kabla kwenye tarehe 15 Juni.  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi karibu na tarehe hii, kuanzia tarehe 14 Juni hadi 16 Juni.  Kwa hiyo kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Lakini lazima ukumbuke kuwa mbegu za kiume zinaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanamke kwa siku 7, kwa hiyo ili kuwa na uhakika Zaidi ya kuepukana na kupata mimba, una takiwa kutokufanya mapenzi kuanzia tarehe 8 hadi 16 Juni.

2. Katika mfano mwingine, kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 13 Juni (na una mzunguko wa hedhi wa siku 28), basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 11 Julai.  Kwa hiyo yai lako litapevuka siku 14 kabla kwenye tarehe 28 Juni.  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi kati ya tarehe 27 Juni na 29 Juni.  Ili kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Kwa usalama zaidi, usifanye mapenzi kuanzia 21 hadi 29 Juni.

3. Katika mfano mwingine, kama baada ya kuandaa kalenda kuonesha mzunguko wako wa hedhi wa miezi 3 hadi 6 iliyopita, unagundua kuwa mzunguko wako ni wa siku 33 badala ya siku 28, basi kifuatacho ni kweli:  kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 1 Juni basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 4 Julai.  Kwa hiyo yai lako litapevuka kwenye tarehe 20 Juni (Siku 14 kabla ya  tarehe 4 Julai).  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi kati ya tarehe 19 na 21 Juni. Ili kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Kwa usalama zaidi, usifanye mapenzi kuanzia 13 hadi 21 Juni.

4. Katika mfano mwingine, kama baada ya kuandaa kalenda kuonesha mzunguko wako wa hedhi wa miezi 3 hadi 6 iliyopita, unagundua kuwa mzunguko wako ni wa siku 26 badala ya siku 28, basi kifuatacho ni kweli:  kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 1 Juni basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 27 Juni.  Kwa hiyo yai lako kitapevuka kwenye tarehe 13 Juni (Siku 14 kabla ya  tarehe 27 Juni).  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi kati ya tarehe 12 na 14 Juni.  Ili kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Kwa usalama zaidi, usifanye mapenzi kuanzia 6 hadi 14 Juni.

Faida ya kutumia njia hiyo
MOJA, Haina madhara yeyote ya kimwili.

Matatizo yanayoweza kujitokeza
MOJA, Njia ya kalenda si kinga dhidi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.
PILI, Njia hii ni ngumu na inahitaji wanawake kuwa wastadi katika hisabati, na kuwa waangalifu sana kuandika au kukumbuka tarehe ya kuanza kipindi chao cha hedhi cha mwisho.

TATU, Huchukua muda mrefu (miezi 3 hadi 6) kufahamu urefu wa mzunguko cha hedhi.
TATU, Mzunguko wa hedhi huweza kubadilika wakati wowote kufuatana na mabadiliko katika mwili.  Hii huweza kusababisha tarehe ya yai kupevuka kuwahi au kuchelewa, kwa hiyo mwanamke huweza kujiweka katika hatari ya kupata mimba bila kufahamu.

NNE, Ili njia hii iwe na uhakika, mwanamke hawezi kufanya mapenzi katika siku zake 9 kila mwezi ambapo kuna uwezekano wa yeye kupata mimba.  Kwa hiyo njia hii inahitaji uwezo mkubwa wa kujidhibiti na hufanya kazi vizuri iwapo mwanaume namwanamke wamekubaliana kufanya hivyo kwa pamoja, na mwanaume anamsaidia mwanamke kuhesabu au kuandika urefu wa mzunguko wake wa hedhi.

TANO, Kwa sababu urefu wa mzunguko wa hedhi wa mwanamke huweza kubadilika ghafla bila kutegemea, hata kama inatumika inavyotakiwa, njia hii si nzuri kama njia nyingine zilizotajwa kuzuia mimba na kupanga uzazi.

Comments

Popular posts from this blog

Aina bora za ng’ombe wa maziwa, banda na namna ya kuanza ufugaji

Uzalishaji wa maziwa ni biashara nzuri sana na ya kuvutia ambayo huwa na faida nyingi na humfanya mfugaji kuridhika hasa kwa yule anayependa kazi hii. Hata hivyo, ni lazima kuanza kwa kuweka msingi imara hata kabla ya kufikiria ni aina gani ya mbegu utaichukua kwa ajili ya kufuga. Ni vizuri kufahamu kuwa, usimamizi ni moja ya jambo muhimu sana ambalo likifanyiwa uzembe linaweza hata kumbadilisha ng’ombe wa maziwa kuwa na uzalishaji duni kama ngo’mbe wa kienyeji. Aina mbalimbali za ng’ombe wa maziwa huwa na mahitaji tofauti, hivyo kiwango cha maandalizi yako ni muhimu sana. Unahitajika kufahamu kuwa, unalazimika kufikia mahitaji yako kwa ajili ya lishe, si kwenye mahitaji ya awali tu bali pamoja na mahitaji ya baadaye ya ngo’mbe wako. Suala hili limefanya wafugaji wengi kushindwa kuendelea kutokana na kuwa hujiingiza katika shughuli hii bila kuangalia mambo ya msingi yanayotakiwa pamoja na kuweka mipango thabiti. Pamoja na kuwa mahitaji yote kwa ajili ya lishe na mambo me...

NAJIVUNIA TANZANIA

ZIJUE HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA NA WAKATI MZURI WA KUTEMBELEA   BAADHI YA HIFADHI ZA TAIFA KATIKA PICHA JINSI ZINAVYOONEKANA Na, Gordon Kalulunga WATANZANIA wengi kutokana na mazoea kuwa wanaotakiwa kutembelea hifadhi za Taifa ni watalii wa nje ya nchi, wameshindwa kujitokeza kwa wingi kutembelea hifadhi hizo kutokana na sababu mbalimbali. Moja ya sababu ya kutoweza kutembelea hifadhi hizo ni pamoja na hofu ya viingilio wakifika katika hifadhi hizo jambo ambalo naamini kuwa baada ya kusoma makala hii wengi wetu tutabadili fikra zetu na kujitokeza katika kutembelea vivutia vya utalii vilivyopo kila pembe ya nchi yetu. Baadhi ya vivutio ambavyo vinasimamiwa kikamilifu na Shirika la Hifadhi za Taifa la Tanzania (TANAPA) ni pamoja na hifadhi ya Taifa ya Arusha, Gombe, Katavi, Mlima Kilimanjaro, Mahale, Mikumi, Manyara, Ruaha, Rubondo, Serengeti, Saadan, Tarangire, Udzungwa, Kitulo, Mkomazi na Saanane. Katika Hifadhi hizo za taifa unapotembelea kuna tozo zak...

How to write a CV: Tips for 2018 (with examples)

When it comes to job hunting, your CV is paramount. Get it right, and you’ll have an interview in no time, but get it wrong, and you may face rejection after rejection. Every CV is different as you want to show why your set of skills makes you suitable for the position you’re applying for at that moment, but all follow a similar structure. This guide will show you how to write a great CV that’s ready for 2018 and beyond. What is a CV? Your CV, short for curriculum vitae ,  is a personal marketing document used to sell yourself to prospective employers. It should tell them about you, your professional history and your skills, abilities and achievements. Ultimately, it should highlight why you’re the best person for the job. A CV is required when applying for a job. In addition to your CV, employers may also require a cover letter and a completed application form( Browse CV templates ) What to include in your CV in 2018 While the structure of a CV is flexible, bending t...