Skip to main content

MAMBO 39 YANAYOWEZA KUKATISHA MAHUSIANO YAKO AU NDOA YAKO

Mambo 39 Yanayovunja Mahusiano Ya Kimapenzi Au Ndoa

1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako.
2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako.
3. Ubishi usiokuwa na maana.
4. Kupenda kujihesabia haki.
5. Kutokubali makosa.
6. Kutokuwa na roho ya msamaha.
7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako.
8. Usaliti wa mapenzi.
9. Kuigiza kupenda.
10. Kutomheshimu mwenzi wako.
11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua.
12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako.
13. Kuwa na jeuri.
14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani. [chumbani]
15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako [ndugu,watoto n.k]
16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja.
17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako [kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako]
18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi.
19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika                maisha yenu.
20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu.
21. Kuwa na ahadi za uongo.
22. Kumdhalilisha mwenzi wako mbele za watu.
23. Kupenda starehe kuliko kuujenga uhusiano wa kudumu [love]
24. Uchafu kutojipenda na kupenda mazingira yako.
25. Maudhi ya mara kwa mara.
26. Kutoonyesha hisia kali hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wako.
27. Kutokuwa karibu na mpenzi wako mara anapokuwa katika msongo wa mawazo.
28. Kutokuwa mbunifu wa maisha mapenzi.
29. Kutokuwa na msimamo katika maamuzi yako [kutoendeshwa na watu]
30. Kutokuwa na muda na mwenzi wako.
31. Kutokuwa na shukrani.
32. Kutokujua gharama za upendo.
33. Kuwa na wivu wa kijinga.
34. Kuwa mbinafsi.
35. Kujifanya kuwa [busy] na kushindwa kumtunza na kumjali mwenzi wako
36. Kutokuwa na imani juu ya mwenzi wako.
37. Kutokubaliana na hali halisi ya maisha yenu.
38. Kutokukubali kujifunza.
39. Kutokutambua maana ya mapenzi na umuhimu wake.

Tabia hizo ndizo zinasababisha mahusiano ya watu wengi kuvunjika, hata ndoa kuharibika maana huyu mtu unayemfanyia hivi ipo siku atachoka, maana hana moyo wa jiwe bali ana moyo wa nyama. Kuvumilia nako kunamwisho wake, hizo tabia ndizo zimechangia maumivu, vidonda vya mapenzi, vifo vya watu wengi na kuwafanya watu wengine kuchukia kupenda na kupendwa katika maisha yao

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO KUMI YA KUFANYA KABLA YA MIAKA 25

1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusagusa.   2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha. 3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwa wazazi au kupanga na nyumba na washkaji. 4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote! 5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi kuu-maintain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana. 6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia. 7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo. 8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza. 9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto. 10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya. Mwajuma huna mpango naye, achana naye. Acha kurudi rudi nyuma!

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 ha...

JE UNAMJUA ALIYETUNGA WIMBO WA TAIFA? HUYU APA

HUYU NDIYE MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA WA TANZANIA JE, unamfahamu mtu aliye tunga sauti (melody ) ya wimbo ambao leo Watanzania wanaiita Wimbo wa Taifa? Huyu ni Enock Sontonga , raia wa Afrika Kusini, aliye tunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ i Afrika’. Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905. Sauti ya wimbo huo u metumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za  Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania ambapo Tanzania na Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii. Nchi zingine tatu za Wazimbabwe , Nami bia na Afrika Kusini imetungwa nyimbo nyingine. Wimbo huu ulitungwa mwaka 1897  na kurekebishwa na wahariri mbalimbali mpaka kufikia kutumika vyema katika maswala ya kitaifa.