Skip to main content

NJIA ZA MAFANIKIO

Miongoni mwa kauli ambazo nilikuwa nasikia wakati nakua nilikuwa nasikia wanasema maisha ni kama kioo ukicheka na yenyewe yanacheka. Kwa kipindi hicho sikuwahi kujua wanamaana gani watu waliyokuwa wanasema hivyo. Ila kwa bahati nzuri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ninavyoelewa walikuwa wanamaanisha nini.

Kwa utafiti wangu nimegundua ya kwamba katika maisha ya kusaka mafanikio ni lazima ujishughulishe kwa kutumia nguvu, kipaji, juhudi na maarifa ili uweze kupata mafanikio hayo. Na endapo utafanya kinyume chache utazidi kulaumu na kuishia kusema ndoto zangu ni kuwa mtu fulani na vitu kama hivyo.

Mwandishi mmoja anayeitwa Charles Nduku aliwahi kuandika katika kitabu chake cha ‘my plan, my life’ kwa kusema acha Kuota ndoto bali anza kufanya.

Kwa kipindi kirefu umekuwa unasema nataka kuwa hivi na vile. Kumbuka ya kwamba huu sio mda wa kusema maneno hayo. Ila muda wakuanza kutekeleza malengo yako. Watu wengi wapo vizuri zaidi kwa kusema kuliko kutenda, na ukichunguza vizuri watu hao hufa na ndoto zao. Badili mtazamo wako na kuwa ni mtu wa vitendo dhidi ya maneno.

Utaweza kubadili mtazamo wako na kuwa mtu wa vitendo ikiwa lakini utajifunza kutumia njia huru za kimafanikio. Kwa kusoma makala haya utajifunza njia hizo huru za mafanikio ambazo zitakufanya ufanikiwe. Naamini una hamu ya kutaka kuelewa ni njia zipi huru za mafanikio ambazo unaweza kuzitumia. Karibu na twende pamoja kujifunza njia hizo.

1. Tafuta nafasi.
Kwa kile ambacho unataka kuwa tafuta nafasi ya kutenda jambo hilo. Watu wengi kama niliposema hapo awali ni wazuri wa kusema kuliko kutenda. Kwa mfano kuna watu wanasema nataka kuwa muigizaji utamsikia akisema tu nataka kuwa muigizaji ila hatafuti nafasi ya kuwa muigizaji. Halikadharika hata wewe mwenye kitu cha tofauti, fanya kitu hicho na usiishie kusema tu haitakusaidia. Endapo utaishia kusema tu jiandae kufa na malengo yako.

Katika kutafuta nafasi ni lazima ujiulize nafasi hiyo ninayo au sina , kama sina naipata wapi? Ni nini kitu ambacho kinahitajika katika nafasi hiyo ninacho au sina kama sina nina kipata wapi? Ukipata majibu ya maswali hayo lazima uweze kufanikiwa.

2. Tengeneza jina.
Katika jambo ambalo unalifanya ni lazima utengeneze jina ambalo watu wataweza kukufahamu kwa kile ambacho unakifanya.

Utengezaji wa jina hutokana na kutengeneza huduma bora kwa watu wengine. Kwa mfano kuna siku nilikuwa katika harakati zangu za hapa na pale nikawa akapita mtoto mdogo ni kamuuliza yule mtoto et nitapata wapi chipsi mtoto yule akanijibu nenda kwa mpemba, wakati najiuliza ni kitu gani kinamfanya huyo mpemba mpaka watoto wadogo wamfahamu, nilipofika hapo kwa huyo mpemba ndipo nilipopata jibu. Ya kuwa ubora na usafi wake ndio uliomfanya atengeneze jina. Jina hilo ndilo linalomtengenezea wataja wengi.

Nadhani pia utakuwa unawafahamu watu wenye majina makubwa ambao wanazalisha vitu vyenye ubora kwa hapa nchini. Kama ndivyo hivyo ni wakati wako na wewe kuweza kutengeneza jina kwa jambo ambalo unalifanya. Ifike wakati mtu akitaka kitu fulani hata ukimuuliza mtu yeyote hata awe mtoto mdogo awe anakufahamu kutoka na kile unachokifanya.

Kama ilivyo leo kwa watu wengi maarufu unaowafahamu..
Ukiyafanya hayo hapo ndipo pesa zitapokuja kwa kasi zaidi. Mbinu hizo huru za kimafanikio wengi waliofanikwa ndizo ambazo walizozitumia. Zitumie leo uwe tajiri mkubwa.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO KUMI YA KUFANYA KABLA YA MIAKA 25

1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusagusa.   2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha. 3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwa wazazi au kupanga na nyumba na washkaji. 4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote! 5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi kuu-maintain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana. 6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia. 7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo. 8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza. 9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto. 10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya. Mwajuma huna mpango naye, achana naye. Acha kurudi rudi nyuma!

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 ha...

JE UNAMJUA ALIYETUNGA WIMBO WA TAIFA? HUYU APA

HUYU NDIYE MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA WA TANZANIA JE, unamfahamu mtu aliye tunga sauti (melody ) ya wimbo ambao leo Watanzania wanaiita Wimbo wa Taifa? Huyu ni Enock Sontonga , raia wa Afrika Kusini, aliye tunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ i Afrika’. Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905. Sauti ya wimbo huo u metumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za  Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania ambapo Tanzania na Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii. Nchi zingine tatu za Wazimbabwe , Nami bia na Afrika Kusini imetungwa nyimbo nyingine. Wimbo huu ulitungwa mwaka 1897  na kurekebishwa na wahariri mbalimbali mpaka kufikia kutumika vyema katika maswala ya kitaifa.