Ndege hatari na mpya zilizotengenezewa kwa teknolojia ya hali ya juu za
F-35 Stealth Fighter Jets tayari zimeruka kutoka jimbo la Utah lililopo
magharibi mwa nchi ya Marekani na kutua UK tayari kabisa kwa training ya
mwisho kuelekea uwanja wa vita.
Ndege hizi ambazo ni mpya na toleo la mwisho limemalizika kutengenezwa
na kujaribiwa March mwaka huu 2017 zinatajwa kuwa ndege hatari zaidi
katika Ground Attacks na Air Defence Missions. Zimepelekwa nchini
Uingereza kwa training ya mwisho kuingia vitani ikiwa na malengo mawili,
moja zitabaki bara la ulaya kulinda uvamizi wa Urusi na pili kupelekwa
uwanja wa vita huko Norh Korea.
Wakati huohuo makamu wa rais wa marekani bwana Mike Pence Leo asubuh
ametembelea ngome (base) ya marekani huko Korea ya kusini ya Camp
Bonifas ambayo iko mpakani kabisa mwa North Korea na South Korea eneo
lenye tension kubwa zaidi na hofu.
Pence amewatoa hofu wananchi wa South Korea kuwa USA iko tayari
kuwalinda na madhara ya vita inayokwenda kutoka muda sio mrefu kwa hiyo
wasihofu kabisa kuhusu usalama wao. Bwana Pence amesema Kim aache kutest
makombora Mara moja na badala yake ayaingize uwanja wa vita kabisa
kuliko mbwembwe za majaribio yasiyofanikiwa. Mike Pence ameziomba jumuia
za kimataifa kuungana na Marekani kuuangamiza kabisa utawala wa
Pyongyang chini ya Dikteta Kim. Hotuba hii ya leo ya Makamu wa Rais
bwana Pence huko Camp Bonifas, South Korea inaonyesha dhahiri kuwa ni
wazi Marekani inakwenda kuivamia kijeshi North Korea muda wowote kuanzia
leo
Source: CNN na NBC News
Comments
Post a Comment