Skip to main content

Posts

Kanuni 29 za kuishi na Watu / Binadam Vizuri Tuesday, August 26, 2017   Makala Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani.  Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani. Zifuatazo ni KANUNI na MBINU mhimu za kuishi na watu vizuri. 1: Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote,hali kadhalika na wewe watakupenda. 2: Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana. 3: Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha       juu na kadhalika. 4: Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu. 5: Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuw

NJIA ZA KUPATA DATA ZILIZOFUTIKA

Njia Za Kupata Data Zako Zilizopotea (Zilizofutwa) Katika Kifaa Cha Android! Aug  2 26 Aug, 2017   Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tulishawahi kufuta taarifa zetu kama vile picha au hata video. Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, TeknoKona inakuletea njia. Sawa kama nlivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye • Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako • Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) yanayofanyikaga automatiki yasifanyike. Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafufua Tuifahamu Njia Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu kinachofuata ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB. Kuna baadhi ya matoleo
likiba awapagawisha mashabiki wake Saturday, August 26, 2017    Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' ambao ameuachia jana amevunja rekodi na kuwapagawisha mashabiki katika mtandao wake wa YouTube katika account yake ya 'Vevo' kutokana na wimbo huo kuwa na kasi kubwa ya watazamaji. Katika mtandao huo ambao Alikiba ameweza kuweka jumla ya video mbili 'Aje Remix' ambayo kwa zaidi ya miezi sita imeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja na kuchangiwa kwa jumla ya 'comment' 1000 huku video yake mpya 'Seducce me' ndani ya masaa 24 imeweza kufikisha watazamaji zaidi ya laki sita na kuchangiwa na watu zaidi ya elfu 6000 ndani ya muda mfupi. Kasi hii si ya kawaida ukilinganisha na video ambayo ipo toka miezi sita iliyopita lakini ni wazi kuwa huenda kasi hii kubwa ya utazamwaji wa video hii unachangiwa na mapokeo mazuri ya washabiki wa muziki wa Alikiba ambao wanajikuta kila wakati wakitaka kuitazama v

INNOVATION CHALLENGE IN MWANZA DTBi,Costech,DLi and BUNI

lEO siku ya ijumaa Vijana karibia 23 ambao wanakuja na aidia nyingi za kutatua changamoto katika jijila Mwanza kuhusu matatizo kama Msongamano wa magari  Uvuvi haramu na Ujangili Ujasiriamali Kilimo Migogoro ya ardhi
TCU Yawatoa Hofu Wanafunzi Wanaotarajia Kujiunga Vyuoni Mwaka Huu   Friday, July 28, 2017   Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa haitegemei kufutiwa udahili kwa wanafunzi kwa baadhi ya vyuo, kutawakosesha baadhi ya wanafunzi watarajiwa nafasi au kozi walizodhamiria kwenda kuzisoma. Akizungumza kwenye Viwanja vya Maonesho, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari Mwandamizi, Edward Mkaku alisema TCU haitahusika na wanafunzi ambao watakosa vyuo kwa sababu kwa sasa wameratibu udahili na hivyo ni jukumu la mwanafunzi kutafuta chuo kulingana na ufaulu alionao. “Hatutarajii mwanafunzi kukosa chuo, na pia kufutiwa udahili kwa baadhi ya vyuo siyo sababu ya wanafunzi kukosa nafasi kwenye vile vyuo vilivyopo,” alisema

CHUKUA TAHADHARII!!!!!!!!!!!

Chukua Tahadhari Kama Unatumia Hizi Bulb   Friday, July 13, 2017     Tunapenda kupunguza matumizi ya nishati, hizi bulb ambazo ni rafiki wa mazingira na zinazookoa nishati(energy serving bulb) zimekuwa zikitumika zaidi kwa sasa. Ila ni vyema ujue kwamba hizi bulb za kisasa ni kweli zina sumu. Shirika la kulinda Mazingira limetoa maelekezo ya dharura unayohitaji kuyafuata endapo bulb yako itavunjika. Hii ni kutokana na gesi yenye sumu inayotoka endapo bulb itavunjika. Taasisi ya Fraunhofer Wilhelm Klauditz ya Ujerumani inadai kuwa kama taa hii itavunjika ndani ya nyumba itatoa  mara 20 zaidi ya Mercury katika hewa Bulb hizi za kupunguza matumizi ya Nishati zinaweza kukuletea matatizo haya; Kizunguzungu Kifafa Maumivu ya kichwa Uchovu Kutostahimili Wasiwasi 1.Bulbu hizi zinazookoa nishati zina wingi wa zebaki(mercury) Mercury ni hatari hasa kwa  watoto na  wanawake wajawazito.  Uharibu mfumo wa neva,  ubongo,  figo na  ini. Pia uharibu uzazi,  kinga ya
  Thursday, July 13, 2017   MABINGWA wa Kombe la SportPesa, Gor Mahia kutoka Kenya wanatarajia kuikaribisha Everton FC inayoshiriki Ligi Kuu England katika mechi ya kirafiki itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam- huku mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wa Tanzania. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, jana aliongoza viongozi mbalimbali wa serikali na wadau wa soka nchini waliojitokeza kuipokea timu hiyo ambayo imekuja nchini kwa mwaliko wa Kampuni ya SportPesa Tanzania. Mechi ya leo itakuwa ni ya kwanza kwa Rooney tangu arejee katika klabu yake hiyo akitokea Manchester United ambayo aliitumikia kwa miaka 13. Kocha wa Everton, Ronald Koeman, alisema kuwa kila mchezaji wa timu hiyo ambaye amekuja nchini atapata muda wa kucheza kuanzia dakika 45 na wataondoka kesho. "Hii ndiyo mechi ya kwanza ya kirafiki na kila mchezaji nitam