Skip to main content

Kanuni 29 za kuishi na Watu / Binadam Vizuri

Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani.

 Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani.

Zifuatazo ni KANUNI na MBINU mhimu za kuishi na watu vizuri.
1: Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote,hali kadhalika na wewe watakupenda.
2: Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana.
3: Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha       juu na kadhalika.
4: Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu.
5: Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe.
6: Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya kumsaidia na              kumjenga.
7: Usiwe msengenyaji na usimseme mtu vibaya.
8: Usipende kugombeza na kutukana au kutoa matusi kwa watu.
9: Shukru kwa kila jambo jema linapotendeka kwa kusema ahsante au shukru kwa kila jambo._
10: Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa.
11: Usipende mabishano na kama yakitokea,usitake kila mara kushinda.
12: Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu.
13: Usipende kugombana,kupiga au kupigana na watu.
14: Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa kwa lolote lile,kama kuna jambo zuri kwako acha wengine         wakusifu.
15: Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki.
16: Usilipize kisasi,badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea.
17: Usiwe unachonganisha watu,ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesema.
18: Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako,ndipo na watu nao watakupenda         na kukubali kama ulivyo.
19: Tunza siri zako na za wengine.
20: Usiwe mwepesi wa hasira
21: Kumbuka majina ya watu unaokutana nao.
22: Usiwe mzungumzaji kupita kiasi,badala yake uwe msikilizaji mzuri.
23: Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli.
24: Zungumza kufuatana na mambo mtu anayoyapenda.
25: Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika.
26: Jifunze kusamehe makosa ya watu.
27: Unapofanya makosa,kubali na kuungama na kuomba msamaha.
28: Heshimu na kuvumilia mawazo na maoni ya wengine ambayo ni tofauti na yako.
29: Nigongee like hata kama hujaipenda hii.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO KUMI YA KUFANYA KABLA YA MIAKA 25

1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusagusa.   2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha. 3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwa wazazi au kupanga na nyumba na washkaji. 4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote! 5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi kuu-maintain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana. 6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia. 7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo. 8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza. 9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto. 10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya. Mwajuma huna mpango naye, achana naye. Acha kurudi rudi nyuma!

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 ha...

JE UNAMJUA ALIYETUNGA WIMBO WA TAIFA? HUYU APA

HUYU NDIYE MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA WA TANZANIA JE, unamfahamu mtu aliye tunga sauti (melody ) ya wimbo ambao leo Watanzania wanaiita Wimbo wa Taifa? Huyu ni Enock Sontonga , raia wa Afrika Kusini, aliye tunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ i Afrika’. Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905. Sauti ya wimbo huo u metumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za  Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania ambapo Tanzania na Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii. Nchi zingine tatu za Wazimbabwe , Nami bia na Afrika Kusini imetungwa nyimbo nyingine. Wimbo huu ulitungwa mwaka 1897  na kurekebishwa na wahariri mbalimbali mpaka kufikia kutumika vyema katika maswala ya kitaifa.