Skip to main content

likiba awapagawisha mashabiki wake

 Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' ambao ameuachia jana amevunja rekodi na kuwapagawisha mashabiki katika mtandao wake wa YouTube katika account yake ya 'Vevo' kutokana na wimbo huo kuwa na kasi kubwa ya watazamaji.

Katika mtandao huo ambao Alikiba ameweza kuweka jumla ya video mbili 'Aje Remix' ambayo kwa zaidi ya miezi sita imeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja na kuchangiwa kwa jumla ya 'comment' 1000 huku video yake mpya 'Seducce me' ndani ya masaa 24 imeweza kufikisha watazamaji zaidi ya laki sita na kuchangiwa na watu zaidi ya elfu 6000 ndani ya muda mfupi.

Kasi hii si ya kawaida ukilinganisha na video ambayo ipo toka miezi sita iliyopita lakini ni wazi kuwa huenda kasi hii kubwa ya utazamwaji wa video hii unachangiwa na mapokeo mazuri ya washabiki wa muziki wa Alikiba ambao wanajikuta kila wakati wakitaka kuitazama video hiyo.

Haya ni baadhi ya maoni ya watu ambao wameweza kuitazama video hiyo na kufunguka ya moyoni mwao

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO KUMI YA KUFANYA KABLA YA MIAKA 25

1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusagusa.   2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha. 3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwa wazazi au kupanga na nyumba na washkaji. 4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote! 5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi kuu-maintain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana. 6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia. 7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo. 8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza. 9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto. 10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya. Mwajuma huna mpango naye, achana naye. Acha kurudi rudi nyuma!

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 ha...

JE UNAMJUA ALIYETUNGA WIMBO WA TAIFA? HUYU APA

HUYU NDIYE MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA WA TANZANIA JE, unamfahamu mtu aliye tunga sauti (melody ) ya wimbo ambao leo Watanzania wanaiita Wimbo wa Taifa? Huyu ni Enock Sontonga , raia wa Afrika Kusini, aliye tunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ i Afrika’. Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905. Sauti ya wimbo huo u metumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za  Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania ambapo Tanzania na Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii. Nchi zingine tatu za Wazimbabwe , Nami bia na Afrika Kusini imetungwa nyimbo nyingine. Wimbo huu ulitungwa mwaka 1897  na kurekebishwa na wahariri mbalimbali mpaka kufikia kutumika vyema katika maswala ya kitaifa.