Skip to main content

Dk Mpango awasilisha taarifa ya Airtel kwa Rais Magufuli

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amewasilisha kwa Rais John Magufuli taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel na kueleza jinsi Serikali ilivyoingizwa mkenge.

Taarifa hiyo imewasilishwa jana baada ya Rais Magufuli kutoa agizo la kufanyika hivyo Desemba 20 mwaka jana.

Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Dk Mpango alisema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kwenda Celtel, baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu.

Kufuatia ukiukwaji huo Dk Mpango amesema Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili nchi iweze kupata haki yake.

“Lakini niwaambie Watanzania yale ambayo tumeyaona ni machafu sana, ni mambo ya hovyo kabisa, nchi yetu kwa kifupi tuliingizwa mkenge, ni fedha nyingi zimepotea kwa hiyo sisi katika majadiliano haya lengo letu litakuwa ni kuhakikisha Watanzania wanapata haki yao,” alisema Dk Mpango.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO KUMI YA KUFANYA KABLA YA MIAKA 25

1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusagusa.   2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha. 3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwa wazazi au kupanga na nyumba na washkaji. 4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote! 5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi kuu-maintain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana. 6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia. 7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo. 8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza. 9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto. 10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya. Mwajuma huna mpango naye, achana naye. Acha kurudi rudi nyuma!

NAJIVUNIA TANZANIA

ZIJUE HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA NA WAKATI MZURI WA KUTEMBELEA   BAADHI YA HIFADHI ZA TAIFA KATIKA PICHA JINSI ZINAVYOONEKANA Na, Gordon Kalulunga WATANZANIA wengi kutokana na mazoea kuwa wanaotakiwa kutembelea hifadhi za Taifa ni watalii wa nje ya nchi, wameshindwa kujitokeza kwa wingi kutembelea hifadhi hizo kutokana na sababu mbalimbali. Moja ya sababu ya kutoweza kutembelea hifadhi hizo ni pamoja na hofu ya viingilio wakifika katika hifadhi hizo jambo ambalo naamini kuwa baada ya kusoma makala hii wengi wetu tutabadili fikra zetu na kujitokeza katika kutembelea vivutia vya utalii vilivyopo kila pembe ya nchi yetu. Baadhi ya vivutio ambavyo vinasimamiwa kikamilifu na Shirika la Hifadhi za Taifa la Tanzania (TANAPA) ni pamoja na hifadhi ya Taifa ya Arusha, Gombe, Katavi, Mlima Kilimanjaro, Mahale, Mikumi, Manyara, Ruaha, Rubondo, Serengeti, Saadan, Tarangire, Udzungwa, Kitulo, Mkomazi na Saanane. Katika Hifadhi hizo za taifa unapotembelea kuna tozo zak...

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 ha...