Skip to main content

Posts

NJIA ZA MAFANIKIO

Miongoni mwa kauli ambazo nilikuwa nasikia wakati nakua nilikuwa nasikia wanasema maisha ni kama kioo ukicheka na yenyewe yanacheka. Kwa kipindi hicho sikuwahi kujua wanamaana gani watu waliyokuwa wanasema hivyo. Ila kwa bahati nzuri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ninavyoelewa walikuwa wanamaanisha nini. Kwa utafiti wangu nimegundua ya kwamba katika maisha ya kusaka mafanikio ni lazima ujishughulishe kwa kutumia nguvu, kipaji, juhudi na maarifa ili uweze kupata mafanikio hayo. Na endapo utafanya kinyume chache utazidi kulaumu na kuishia kusema ndoto zangu ni kuwa mtu fulani na vitu kama hivyo. Mwandishi mmoja anayeitwa Charles Nduku aliwahi kuandika katika kitabu chake cha ‘my plan, my life’ kwa kusema acha Kuota ndoto bali anza kufanya. Kwa kipindi kirefu umekuwa unasema nataka kuwa hivi na vile. Kumbuka ya kwamba huu sio mda wa kusema maneno hayo. Ila muda wakuanza kutekeleza malengo yako. Watu wengi wapo vizuri zaidi kwa kusema kuliko kutenda, na ukichunguza vi

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA BIASHARA

Njia pekee itakuyokusaidia kuingiza kipato cha ziada na kukupeleka kwenye uhuru wa kifedha ni kwa wewe kuamua kuanzisha biashara yako na utakayoamua kuisimamia kikamilifu hadi ikuletee mafanikio. Ili kuanzisha biashara na ikafika mahali ukaanza kuona matunda ya biashara yako, kwa kawaida huwa ipo misingi au mambo ambayo unatakiwa uzingatie sana ili biashara yako iweze kudumu na kutoa faida uitakayo. Yafuatayo Ni Mambo Ya Kuzingatia Pale Unapoanzisha Biashara.  1. Elewa wateja wako wa mwanzo wanataka nini na hapo utapata picha ya jinsi utavyoiendesha biashara na uzingativu juu ya kazi. Ukijua wateja wako wanataka kitu gani, itakusaidia sana kuweza kuwapa huduma hiyo. 2. Kuwa mbunifu,  hilo ndilo jambo kubwa zaidi, biashara ni zilezile ila kinachofanya wateja wakimbilie biashara  yako ni ubunifu wako. Kama usipokuwa mbunifu na ukataka kufanikiwa kibiashara uwe na uhakika utakwama. 3. Lugha nzuri kwa wateja na ukarimu, huweza kumasisha kuongezeka wa wateja wengi kati

ATHARI ZA UVUTAJI WA SIGARA

Assalaamu Alaykum wasikilizaji wapenzi na karibuni kutegea sikio kipindi kingine cha Ijue Afya Yako. Leo tutazungumzia madhara ya kuvuta sigara, tabia ambayo imezoeleka na watu wengi ingawa ina madhara mengi. Ili kuweza kuyajua madhara hayo kwa undani, usiondoke kando ya redio yako hadi mwisho wa kipindi hiki. Kemikali zenye madhara zilizo kwenye sigara Ufutaji sigara huathiri mwili kwa njia tofauti na madhara yake ni makubwa kiafya. Inakadiriwa kuwa, hadi sasa kumegunduliwa kemikali zipatazo 7,000 katika moshi wa sigara ambapo 250 kati ya hizo ni sumu na 70 zinasababisha kansa. Mvutaji mdogo hutumia nusu ya pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa mwaka. Mada na kemikali zilizo kwenye sigara huathiri karibu kila kiungo mwilini kuanzia seli hadi mfumo wa kulinda mwili. Kemikali zilizoko kwenye moshi wa sigara huingia katika mapafu na kuenea katika mwili mzima na kusababisha madhara makubwa kwa njia mbalimbali. I

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6.  Hii itamsaidia kujua l

MAREKANI WAFYATA MKIA KWA KOREA

Marekani iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini yenye lengo la kuondoa zana za nuklia kutoka eneo hilo, Kauli hiyo ni kwa mjibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson. Lakini amesema kuwa Marekani itatumia nguvu za kijeshi ikiwa itahitajika. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa China, mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini, anasema makubaliano ya amani ndio njia pekee. Bwana Tillerson aliliambia baraza la ulinza la Umoja wa Mataifa kuwa tisho la Korea Kaskazini la kushambulia majirani zake na zana za nuklia. Maelfu ya wanajeshi wa Marekani wako nchi majirani wa Korea Kaskazini ikiwemo Korea Kusini na Japan. Tillerson amezitaka nchi wachama wa Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo na kupunguza uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi hiyo. "Kwa miaka kadha Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha kwa nguvu mpango huu hatari." "Ni wakati wetu kuchukua hatua na kudhibiti hali," Tisho la Korea Kaska

FAIDA YA KUWATHIMINI WAFANYAKAZI WA NDANI MAJUMBANI NA MADHARA YANAYOWEZA TOKEA IKIWA WATATESWAWA WATA

Kumekuwa na matukio mbalimbali yanatokea yakihusu wafanyakazi au wasaidizi wa kazi za ndani. Matatizo mengi yanatokea katika familia nyingi hayaji tu kama radi lazima kuna sababu zinazopelekea kutokea kwa matatizo hayo. Huwezi kupanda mahindi shambani halafu ukategemea kuvuna mbaazi. Hivyo siku zote utavuna kile ulichopanda. Kama ukipanda mbegu bora ya upendo katika familia yako tegemea kuvuna mbegu bora ya upendo. Vivyo hivyo, kama ukipanda chuki katika familia yako tegemea kuvuna mauti. Hii ni sheria ya asili unapokea kile unachotoa. Kwa tafiti zisizo rasmi, ukitembelea nyumba kumi kati ya nyumba hizo kumi moja tu ndio wanaishi vema na wasaidizi wao wa kazi za ndani. Nyumba nyingi ni matatizo sana je matatizo haya yote yanasababishwa na nani? Lazima tuchunguze nini kiini cha kosa au tatizo kwanza. Huwezi kutatua tatizo bila kuchunguza kiini cha kosa. Visa vimekuwa vikitawala ndani ya nyumba nyingi kwa wale wanaoishi na wasaidizi wao wa kazi za ndani. Wasaidizi wa

MAMBO 39 YANAYOWEZA KUKATISHA MAHUSIANO YAKO AU NDOA YAKO

Mambo 39 Yanayovunja Mahusiano Ya Kimapenzi Au Ndoa 1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako. 2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako. 3. Ubishi usiokuwa na maana. 4. Kupenda kujihesabia haki. 5. Kutokubali makosa. 6. Kutokuwa na roho ya msamaha. 7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako. 8. Usaliti wa mapenzi. 9. Kuigiza kupenda. 10. Kutomheshimu mwenzi wako. 11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua. 12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako. 13. Kuwa na jeuri. 14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani. [chumbani] 15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako [ndugu,watoto n.k] 16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja. 17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako [kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako] 18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi. 19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika                maisha yenu. 20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu. 21. Kuwa na ahadi za uongo.