Skip to main content

NJIA ZA KUWA MFANYA BIASHARA MKUBWA

ifuatazo Ndizo Njia 7 Za Kuwa Mafanyabiashara Mkubwa

1. Chagua wazo bora la kibiashara.
Wazo bora la kibiashara ndilo litakalo kufanya kuwa mfanyabiashara wa mkubwa. Mara nyingi nimekuwa nikikutana na watu wakisema wanataka kuwa wafanyabiashara na kuishia kusema tu. Ila ukweli ni kwamba katika kuchagua wazo bora la kibiashara ni lazima ujiulize je unataka kuwa mzalishaji wa bidhaa au huduma? Je unataka kuwa mnunuzi na muuzaji?au  je unataka kuwa msambazaji tu ? Hayo yanaweza kuwa miongoni mwa maswali ya msingi ya kujiuliza.

2. Fanya uchunguzi juu ya washindani wako.
Hapa ndipo jicho la tatu linaposhindwa kufanya kazi mara nyingi. Tumekuwa si wachunguzaji wazuri juu ya washindani wetu ila tumekuwa wasikilizaji tu kwa watu wengine juu ya washindani wetu. Ila ikumbukwe ya kwamba fanya uchunguzi wa kutosha ili kujua washindani wako wanatumia mbinu zipi kukuza biashara zao. Hii itakusadia pia kujua ni wapi wanapokosea ili uweze kulizipa pengo hilo. Kwa kufanya hivi kutakufanya ndoto zako za kuwa mfanyabiashara wa kimataifa zitimie.

3. Tafuta mtu wa kukuongoza. (Helpful mental).
Tafuta mtu sahihi wa kukuongoza  na si mtu wa kukukwamisha. Watu wengi tunashindwa kuwa wafanyabishara wakubwa hii ni kutokana tunatafu watu ambao sio sahihi katika kutushauri. Stuka mapema juu ya jambo hili. Na anza kukaa na watu ambao tayari wamefanikiwa kwenye biashara zao watakusaidia sana kufika kule unakotaka kufika kibiashara. Siku zote ukitaka kuruka kama tai, ni lazima ujifunze kama tai wanavyoruka. Kwa maana huyo ukitaka kuwa mfanyabiashara mkubwa kubali kuchukua mwongozo wa wafanyabiashara waliofanikiwa.

4. Tambua biashara inayokua.
 Ukilijua hili ni jambo jema zaidi. Moja ya tatizo kubwa ni kwamba tumekuwa tukishuhudia biashara hazikuwi miaka nenda miaka rudi. Hii ni sababu kubwa ambayo inachangia tusiweze kujua ni kwa jinsi gani tusiwe wafanyabiashara wakubwa. Natamani kuona malengo yako yanabadilishwa kila wakati. Kwa mfano leo unauza nguo kwa kutembeza, ili kuona biashara inakuwa tunataka kuona unapata chumba kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo napo kweli tunasema biashara inakua. Kama unafanya biashara mkoa wako mzima tunatamani kuona unaongeza mkoa mwingine na mwingine katika kusambaza huduma au bidhaa.

5. Panga malengo na mipango ya biashara yako.
Hapa inahusiana na juu ya kuuza, kununua bidhaa au huduma. Lazima malengo ya biashara yako uyapange kila robo ya mwaka ili kugundua kama biashara yako inakuwa au haikui. Na lazima pia katika kupanga malengo yako, utambue baada ya muda fulani biashara yako itakuwa imefika wapi. Kwa mfano ni muhimu kujua biashara yako itakapokuwa baada ya miaka miwili au mitatu mbeleni.

6. Tangaza biashara yako.
Wateja wako ni lazima wajue bidhaa na huduma ambayo unazalisha. Si kujua tu, lengo jingine la kutangaza bidhaa au huduma inamfanya mtumiaji aweze kujua jinsi ya kutumia kitu hicho. Kwa kutangaza biashara wateja huongezeka kwa asilimia kubwa sana na kufanya huduma au bidhaa yako kuweza kupendwa na wengi pia. Matangazo ni njia mojawapo bora ya kukufanya kuwa mfanyabiashara wa kimataifa ikiwa utaitumia vizuri.

7. Jenga mahusiano mazuri na wateja wako.
Jitahidi kulizingatia hili ya kwamba Kauli katika biashara ni mali kuliko hata  pesa. Jali wateja wako na kuwafanya wajihisi kama wanapata bidhaa bure. Kwa kadri utakavyozidi kujenga mahusiano bora na wateja hiyo itapelekea wao kupenda bidhaa zako na hiyo itakusaidia kukuza wateja wengi siku hadi siku.

Ni matumaini yangu umenielewa vizuri hizo ni baadhi ya siri chache kati nyingi zitakazokufanya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Asante sana na usisite kumshirikisha mwingine.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO KUMI YA KUFANYA KABLA YA MIAKA 25

1. Jifunze kuweka akiba ya fedha na iache bila kuigusagusa.   2. Tafuta mpenzi sahihi na tulia naye, panga maisha. 3. Ishi mahali pa peke yako, acha kuishi kwa wazazi au kupanga na nyumba na washkaji. 4. Lipa madeni yako ya zamani. Yote! 5. Tengeneza mwili ambao unataka halafu jitahidi kuu-maintain! Anza kuzingatia kuishi kwa kujali afya yako sana. 6. Jitahidi uwe na marafiki ambao wana changamoto za kimaendeleo zitakazokusaidia. 7. Anza kujinunulia assets kama ardhi na nyinginezo. 8. Jifunze kuvaa vizuri na kwa heshima, si tu ilimradi umependeza. 9. Kubali sasa kwamba umekua na acha tabia na mambo ya kitoto. 10. Yaache ya zamani yapite na anza mapya. Mwajuma huna mpango naye, achana naye. Acha kurudi rudi nyuma!

JE UNAMJUA ALIYETUNGA WIMBO WA TAIFA? HUYU APA

HUYU NDIYE MTUNZI WA WIMBO WA TAIFA WA TANZANIA JE, unamfahamu mtu aliye tunga sauti (melody ) ya wimbo ambao leo Watanzania wanaiita Wimbo wa Taifa? Huyu ni Enock Sontonga , raia wa Afrika Kusini, aliye tunga mashairi ya wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha moja ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ i Afrika’. Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905. Sauti ya wimbo huo u metumiwa na nchi kadhaa kwa nyimbo za taifa za  Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Zambia na Tanzania ambapo Tanzania na Zambia zimeendelea kuitumia ‘melody’ hiyo hadi leo hii. Nchi zingine tatu za Wazimbabwe , Nami bia na Afrika Kusini imetungwa nyimbo nyingine. Wimbo huu ulitungwa mwaka 1897  na kurekebishwa na wahariri mbalimbali mpaka kufikia kutumika vyema katika maswala ya kitaifa.

JIFUNZE KALENDA YA UZAZI

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6.  Hii itamsaidia kujua l