Tanzania nchi ya amani ndugu zangu tudumixhe upendo amani na mshikamano mambo yasiyo ya msingi tusiyaweke mbele tufanye kazi ndoto haziwezi kutimia kwa kukaa na kulia lia mtaani onyesha jitume tusikalie mitandao tunawafaidisha wenzetu huku sisi tukiludi nyuma "nawapenda watanzania wenzangu tufanye kazi tusonge mbele"
Uzalishaji wa maziwa ni biashara nzuri sana na ya kuvutia ambayo huwa na faida nyingi na humfanya mfugaji kuridhika hasa kwa yule anayependa kazi hii. Hata hivyo, ni lazima kuanza kwa kuweka msingi imara hata kabla ya kufikiria ni aina gani ya mbegu utaichukua kwa ajili ya kufuga. Ni vizuri kufahamu kuwa, usimamizi ni moja ya jambo muhimu sana ambalo likifanyiwa uzembe linaweza hata kumbadilisha ng’ombe wa maziwa kuwa na uzalishaji duni kama ngo’mbe wa kienyeji. Aina mbalimbali za ng’ombe wa maziwa huwa na mahitaji tofauti, hivyo kiwango cha maandalizi yako ni muhimu sana. Unahitajika kufahamu kuwa, unalazimika kufikia mahitaji yako kwa ajili ya lishe, si kwenye mahitaji ya awali tu bali pamoja na mahitaji ya baadaye ya ngo’mbe wako. Suala hili limefanya wafugaji wengi kushindwa kuendelea kutokana na kuwa hujiingiza katika shughuli hii bila kuangalia mambo ya msingi yanayotakiwa pamoja na kuweka mipango thabiti. Pamoja na kuwa mahitaji yote kwa ajili ya lishe na mambo me...
Comments
Post a Comment