Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2017
Kanuni 29 za kuishi na Watu / Binadam Vizuri Tuesday, August 26, 2017   Makala Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani.  Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani. Zifuatazo ni KANUNI na MBINU mhimu za kuishi na watu vizuri. 1: Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote,hali kadhalika na wewe watakupenda. 2: Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana. 3: Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha       juu na kadhalika. 4: Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu. 5: Uwe mcheshi na mtu am...

NJIA ZA KUPATA DATA ZILIZOFUTIKA

Njia Za Kupata Data Zako Zilizopotea (Zilizofutwa) Katika Kifaa Cha Android! Aug  2 26 Aug, 2017   Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tulishawahi kufuta taarifa zetu kama vile picha au hata video. Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, TeknoKona inakuletea njia. Sawa kama nlivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye • Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako • Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) yanayofanyikaga automatiki yasifanyike. Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafufua Tuifahamu Njia Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu kinachofuata ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB. Kuna baadhi ya...
likiba awapagawisha mashabiki wake Saturday, August 26, 2017    Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' ambao ameuachia jana amevunja rekodi na kuwapagawisha mashabiki katika mtandao wake wa YouTube katika account yake ya 'Vevo' kutokana na wimbo huo kuwa na kasi kubwa ya watazamaji. Katika mtandao huo ambao Alikiba ameweza kuweka jumla ya video mbili 'Aje Remix' ambayo kwa zaidi ya miezi sita imeweza kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja na kuchangiwa kwa jumla ya 'comment' 1000 huku video yake mpya 'Seducce me' ndani ya masaa 24 imeweza kufikisha watazamaji zaidi ya laki sita na kuchangiwa na watu zaidi ya elfu 6000 ndani ya muda mfupi. Kasi hii si ya kawaida ukilinganisha na video ambayo ipo toka miezi sita iliyopita lakini ni wazi kuwa huenda kasi hii kubwa ya utazamwaji wa video hii unachangiwa na mapokeo mazuri ya washabiki wa muziki wa Alikiba ambao wanajikuta kila wakati wakitaka kuitazama v...