Dk Mpango awasilisha taarifa ya Airtel kwa Rais Magufuli Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amewasilisha kwa Rais John Magufuli taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel na kueleza jinsi Serikali ilivyoingizwa mkenge. Taarifa hiyo imewasilishwa jana baada ya Rais Magufuli kutoa agizo la kufanyika hivyo Desemba 20 mwaka jana. Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Dk Mpango alisema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kwenda Celtel, baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu. Kufuatia ukiukwaji huo Dk Mpango amesema Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili nchi iweze kupata haki yake. “Lakini niwaambie Watanzania yale ambayo tumeyaona ni machafu sana, ni mambo ya hovyo kabisa, nchi yetu kwa kifupi tuliingizwa mkenge,...
This is Blog aim at give the update information on the real life and leads to acknowledge the individual with the knowledge and skills on the different phenomena like technology, business, education and relationship